Mwafrika wa kwanza ashinda taji la UFC

 Mwanamasubwi wa Nigeria Kamaru Usman ameandikisha historia ya kuwa mwanamasumbi wa kwanza wa Afrika kushinda taji Ultimate Fighting Championship (UFC). 

Mwanamasubwi huyo amempiga mmarekani Tyron Woodley mjini Las Vegas katika shindano la uzani wa welterweight. 

Taji la UFC ilinahusisha mashiindano ya mchanganyiko wa ndondi, mateke, jiu-jitsu, mieleka na michezo mingine ambapo wachezaji wanapigana katika eneo maalum bila viatu. 

Usman, 31, alifanya vizuri katika mashindo hayo baada ya kumuondoa kileleni nyota wa miaka mingi wa taji hilo Woodley. 


Aliimarisha ushindi wake kwa alama 14 na kuweka rekodi ya kutoshindwa katika mashindano ya UFC. 

Baada ya mashindano hayo Usma alifichua kwa waandishi wa habari kuwa alivunjika mguu wiki moja kabla ya kinyang'nyiro hicho. 

Alianza kwa kuwasalimia wanahabari kwa lugha ya kiarabu kisha akabadilisha kwa lugha ya Pidgin. 

"Nigeria, niliwaambia kuwa tutashinda taji hili, niliwaahidi kuwa sitawafeli na leo tumefanya hivyo," alisema kwa kipidgin. 

Usman alizaliwa Nigeria, lakini wazazi wake walihamia Arlington katika jimbo la Texas akiwa mdogo. 

Miaka 23 baadae najivunia jina la utani la ''Nigerian Nightmare'' aliimbia BBC. 

Lakini anaafiki kuwa si yeye pekee mwanamichezo anayetambulika kwa jina hilo. 

Aliwaita jukwaani mwanamasumbwi mwingine kutoka nchini mwake kama vile Samuel Peter na mkuu wa kandanda katika mji wa Kansas, Christian Okoye. 

Usman, alianza mchezo wa mieleka akiwa shule ya upili akiwa Texas na aliendelea kushiriki mchezo huo hadi wa leo. 

"Wakati umewadia kubadilisha hali yangu siyo mieleka pekee tena, lakini nataka kuandikisha historia katika ulingo huo nijikimu kimaisha na kusaidia familia yangu pia," aliiambia BBC michezo. 

Wachezaji kama Usman ambao wameshiriki shindano la UFC kutoka kwa michezo mingine hupata umaarufu mkubwa. 

No comments

Powered by Blogger.