Cristiano Ronaldo achukuliwa hatua na Uefa kwa 'kushangilia' bao


Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo amechukuliwa hatua za kinidhamu na Uefa baada ya kushangilia 'visivyo' ushindi wa klabu yake dhidi ya Atletico Madrid katika mchuano wa ligi ya mabingwa wa kufuzu kwa awamu ya robo fainali juma lililopita. 

Nyota huyo wa 34 alionekana kumkejeli meneja wa Atletico, Diego Simeone, huku akiwageukia mashabiki wa klabu hiyo na kujishika sehemu zake za siri. 

Ronaldo alifanya kosa hilo wakati akishangilia hat-trick yake iliyoifanya Juventus kuishinda Atletico mabao 3-0, Uefa itatoa uamuzi wa kesi hiyo Machi 21. 

No comments

Powered by Blogger.