Binadamu wa kwanza kukanyaga katika sayari ya Mihiri "Mars" anatarajiwa kuwa mwanamke

Taasisi inayojihusisha na utafiti wa masuala ya anga nchi Marekani NASA imetangaza kwamba binadamu wa kwanza atakayekanyaga katika sayari ya Mihiri "Mars" anaweza akawa mwanamke . 

Rais wa NASA Jim Bridenstine,akiongea katika kipindi kimoja cha redio alichoshiriki alisema kuna uwezekano binadamu wa kwanza atakayekanyaga katika sayari ya Mihiri akawa mwanamke. 

Bridenstine alisema bado haijaamuliwa ni mtu gani ataenda katika sayari ya Mihiri, alifahamisha kwamba mipango yao kwa siku zijazo ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu na kuwa mstari wa mbele. 

Bridenstine, alimjibu shabiki mmoja aliyemuuliza kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kama katika safari ya mwezi ujao ya NASA kutakuwa na nafasi kwa wanawake , kwa kusema “bila shaka” 

 NASA  kwa mara ya kwanza ipo katika maandalizi ya kumpeleka mwanamke katika anga za mbali.

No comments

Powered by Blogger.