Wanafunzi watoro kutoruhusiwa kufanya mitihani

 Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar, Riziki Pembe Juma amesema Wizara ya Elimu imeandaa mikakati maalum  ya kutowaruhusu kusajiliwa kufanya mitihani wanafunzi ambao watoro, mikakati huo una lengo la kupunguza matokea mabaya kwa skuli za Zanzibar. 

Aliyaeleza hayo wakati akizindua kampeni ya 'Tukutane Skuli' yenye lengo la kushajihisha wanafunzi kusoma, 

Waziri huyo alisema kuwa utoro wa wanafunzi unapelekea kusababisha Zanzibar kutoa baadhi ya skuli kuwa ni miongoni mwa skuli za mwisho katika mitihani ya taifa. 

“Tumebaini kuwa utoro ndio uliokuwa unapelekea Zanzibar kupata matokeo mabaya katika mitihani mbali mbali ikiwemo kidato cha nne na sita,”alieleza waziri. 

Alisema  kwasasa wizara hiyo imeweka mikakati maalum ya kupambana na matokeo mabaya ambapo moja ya mkakati ndio huo wa kutowasajili wale watakaobainika kuwa watoro. 

Hata hivyo alitoa wito kwa  walimu kulisimamia suala la utoro ili malengo waliyojiwekea ya  kutokuwa na zero katika matokeo ya mitihani ya taifa ya kidato cha pili,nne na sita yaweze kufikiwa. 

Katika hatua nyengine Waziri Riziki aliwataka  wadau wa Elimu nchini kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kusaidia sekta ya elimu ili kuongeza idadi ya ufaulu kwa wanafunzi. 
Mkuu wa mkoa wa mjini Ayoub Mohammed Mahmoud alisema kupitia taasisi hiyo ataendelea kusaidia na kuunga mkono maendeleo ya sekta ya elimu katika Mkoa huo ili kuona Mkoa wake nunazidi kupata matokeo mazuri katika mitihani ya taifa na hata kuzipita skuli za Tanzania bara. 

Aliongeza kuwa ataendelea kusaidia kambi za wanafunzi wanajitayarisha kwa mitihani kwa skuli mbali mbali za Mkoa wa mjini Magharibi ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika mitihani ya taifa. 

Nae mratibu wa programu ya tukutane skuli Nd Yussuf Mohammed alisema mpango huo ulianza kufanyika  kimkoa kwa skuli kumi za Mkoa wa Mjini Magharibi na utafanyika kitaifa kwa Mikoa yote mitano ya Zanzibar na kila mkoa utahusisha skuli kumi. 

No comments

Powered by Blogger.