Mambo yanayosababisha usikamilishe kazi zako kwa wakati
Hakuna mtu anayependa kushindwa kukamilisha kazi au kitu alichokianza kukifanya, kila mmoja wetu anapenda kuona kila kitu anachokifanya kinakamilika. Hata hivyo mara nyingi kutokukamilisha kazi hutokea kwa watu wengi. Ni ukweli usiopingika kuwa zipo sababu kadha wa kadha zinazosababisha tatizo hili.
Karibu nikufahamishe vitu viwili vinavyokufanya usikamilishe kazi zako kama ifutavyo:
Marafiki au wafanyakazi wengine
Inawezekana unafanya kazi kwenye ofisi au katika eneo ambalo umezungukwa na marafiki zako. Kwa njia moja au nyingine wafanyakazi wenzako au marafiki zako wanaweza kukuzuia kukamilisha kazi zako.
Kwa mfano ukiwa uko ofisini na ukaanza mazungumzo na mfanyakazi mwenzako, ni wazi kuwa utapoteza muda mwingi wa kazi.
Inawezekana pia una rafiki anayekushawishi kufanya mambo kama vile kumsindikiza kwenye matembezi au kukuingiza kwenye mazungumzo na shughuli nyingine ambazo hazihusiani na kazi zako. Moja kwa moja unaona jinsi ambavyo unaweza kupoteza muda mwingi ambao ungeweza kuutumia kukamilisha kazi zako.
Kutokuwa na vipaumbele
Kwa hakika kuna vitu vingi vya kufanya kwa siku. Lakini ili uweze kuvikamilisha vyema huna budi kuweka mpangilio mzuri kwa kutegemea umuhimu kwa kila kitu.
Kuwa na vipaumbele kutakuwezesha kufahamu ni kazi ipi ianze na ifanyike kwa muda gani badala ya kufanya lolote linalokuja tu mbele yako.
Jambo muhimu ili kuepuka kutokamilisha kazi kwa wakati ni kujifunza kusema hapana kwa mambo au watu ambao wanaweza kukupotezea muda na kukufanya usikamilishe lengo lako. Kumbuka kuwa kutumia muda vyema ni msingi wa mafanikio katika jambo lolote.

Post a Comment