Wanafunzi watengeneza koti linaloweza kuzuia mtu kuvamiwa


Wanafunzi wanne kutoka Mexico wametengeneza koti ambalo wanadai linaweza kuzuia mtu kuvamiwa. 

Mikono ya koti hilo linaweza kutoa mshtuko wa umeme utakaomfanya mtu yeyote aliyeligusa kushindwa kutoka. 

Wanafunzi hao waliobaini mbinu ya kuwakamata wavamizi wa kijinsia na wamesema walikuja na wazo hilo baada ya kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu wanaofanyiwa shambulio la kijinsia katika mji wao. 

Aidha wanafunzi hao wamedai kwamba mshtuko huo wa umeme waliouweka kwenye koti ni mdogo hivyo hauwezi kuainishwa kama silaha licha ya kwamba ni imara kuweza kushambulia mtu yeyote. 

Koti hilo linaloitwa women wearable lilitengenezwa na Anaid Parra Quiroz na Esthela Gómez ambao ni wanafunzi wa uhandisi na kushirikiana na Giwan Park ambaye ni mwanafunzi wa kutengeza roboti na mwanafunzi wa sheria ambaye ni Guadalupe Martínez. 

Wanafunzi hao wanne katika chuo cha Puebla walikuja na wazo hilo ikiwa ni sehemu ya ujasiriamali darasani. 

Mamlaka ya mji huo wa Puebla umetoa takwimu zinaonyesha kuwa uvamizi wa kingono unaripotiwa mara tatu kila siku. 

Ni namna gani koti hilo linafanya kazi? 
Wanafunzi hao walinunua kitambaa cha aina ya kotoni na kuweka ndani betri aina ya 9v katikati ya kitambaa cha ndani na nje,waya hizo zilifungwa vizuri ili lisiweze kumdhuru mvaaji ,vilevile kuna kifungo ambacho unaweza kuwasha na kuzima mtambo huo kwenye koti. 

Giwan Park alibuni namna ambavyo mtu anaweza kubonyeza kitufe ambacho lialifanya koti hilo lifanye kazi. 

Wakati ambapo koti hilo linaweza kumdhuru mtu ni wakati ambapo mtu anapogusa koti hilo katika mikono wakati mtu anatembea hivyo mshtuo huo wa umeme unaweza kumpata mtu yeyote atayegusa. 

Wazo hili liko hivyo ili kumpa nafasi aliyevaa koti muda wa kukimbia au kuwasha kengele 

Mwanafunzi wa sheria Guadalupe Martínez aliingia katika utengenezaji wa 'Woman wearable' ili kuhakikisha kuwa hawataenda kinyume na sheria kwa sababu ni chombo cha mtu kujitetea. 

Mshtuo huo wa koti ni mdogo hivyo hauwezi kuhatarisha maisha ya mtu yeyote hivyo haijaweza kufikia kiwango cha kuwa silaha. 

Koti hilo lilichukua miezi mitatu kulitengeneza .Wanafunzi hao wanasema wangependa kuweka chombo hicho katika maeneo mengine ya koti zaidi ya kwenye mikono. 

Hata hivyo chombo hicho kimetengenezwa namna ambavyo inaweza kuwekwa kwenye blause,sketi au suruari. 

Wanafunzi wanasema koti hilo linaweza kuuzwa kwa dola 50 au yuro 40.

No comments

Powered by Blogger.