Tanasha atahadharishwa kuhusu penzi la Diamond na familia yake


Mahusiano kati ya Diamond Platnumz na Tanasha kila kukicha yanazidi kugonga vichwa vya habari, toka mwisho mwa mwaka jana yamekuwa yakichukua nafasi kubwa kwenye mazungumzo mtandaoni. 

Kwa sasa ni mwigizaji wa filamu Bongo, Mwijaku ambaye amemueleza Tanasha kuwa asichukulie kitendo cha kutambulishwa kwa wazazi wa Diamond ndio tayari kaolewa kwani muimbaji huyo sio muoaji na ameshafanya hivyo mara kadhaa. 

"Kutambulishwa sio ndoa, jiulize wangapi wametambulishwa kwa mama yake Diamond. Huu ni 
utamaduni wetu wa Afrika ukitaka kuuteka moyo wa mwanamke mtambulishe kwa wazazi wako," Mwijaku ameiambia Wasafi TV. 

Mwishoni mwa wikiendi iliyopita Diamond na Tanasha waliibua  gunzo mara baada ya kusambaa kwa video mtandaoni ikionyesha Bibie akiwa na mama mzazi wa muimbaji huyo na dada yake, Esma Platnumz. 

No comments

Powered by Blogger.