Vanessa Mdee atia mguu sakata Diamond Platnumz na Rayvanny kufungiwa



Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amesema kuwa anamsapoti Diamond Platnumz na Rayvanny na amewataka kutokata tamaaa katika kipindi wanachopitia. 

Vanessa amesema kuwa wasikate tamaa mwaka huu na unapokuja mwaka 2019 wasikate tamaa pia na hata walivyoomba msamaha katika mitandao ya kijamii aliona pia. 

"Kwanza wote wawili i support them so much, na wasihi wasikate tamaa isiwarudishe nyuma kwa chochote kile walichokipanga mwaka 2019 even 2018, kiukweli niliona appology waliyoipost leo, kila mtu anakuaga katika kipindi anachofanya kazi kwa bidii anajua nguvu ya kufanya kazi kwa bidii na anawekeza na anajua ile nguvu ya kufanya kazi kwa bidii," alisema Vanessa. 

"Najua waliwekeza kwenye ile project, Kwa Basata kuwasimamisha au kuwasitisha kama mimi msanii ningepata mshtuko."

No comments

Powered by Blogger.