Ulimwengu asajiliwa na wapinzani wa Simba

Mshambuliaji wa Tanzania Thomas Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya JS Saoura ya Algeria. 

Ulimwengu amesaini mkataba huo leo ambapo klabu yake hiyo ipo miongoni mwa timu 16 zilizoingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika sambamba na Simba SC ya Tanzania. 

Usajili huu wa Ulimwengu umekuja ikiwa ni miezi miwili tu imepita tangu avunje mkataba na klabu ya Al Hilal ya Sudan ambayo hata hivyo hakuweka wazi sababu za kuvunja mkataba na timu hiyo ndani ya miezi mitatu tu. 

Klabu ya JS Saoura imethibitisha usajili huo kwa kuweka picha ya Ulimwengu akiwa na mabosi wa timu hiyo akikabidhiwa jezi tayari kwa kukipiga.

No comments

Powered by Blogger.