Ambokile awaburuza Makambo, Okwi na Kagere

Mshambuliaji wa timu ya Mbeya, City Eliud Ambokile leo amefikisha bao lake la 9 kwenye ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya African Lyon mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya. 

Ambokile amezidi kuonyesha umahiri wake wa kucheka na nyavu na kuwaacha washambuliaji wa Simba na Yanga Herieter Makambo, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere ambao ni wageni. 

Makambo, Okwi na Kagere wote wana mabao 7 baada ya kucheza mechi 13 kwenye ligi kuu huku Mbeya City wakiwa wamecheza michezo 15.

No comments

Powered by Blogger.