Serikali yawataka wahitimu kuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika Jamii
Wahitimu wa kozi mbalimbali kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wametakiwa kuwa chachu ya kuleta mabadiliko katika Jamii kutokana na elimu waliyoipata kutoka katika Taasisi hiyo.
Hayo yamebainika wakati wa Hotuba ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa Mahafali ya Nane ya Taasisi ya Maendeleo Tengeru kwa wahitimu kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wanapaswa kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii kwa kuhamasisha wananchi kushirikiana na Serikali kujiletea mabadiliko kwa kutumia nguvu zao kufanya kazi na kuacha fikra hasi za kutegemea Serikali kuwafanyia kila kitu.
Naibu Waziri Ndugulile ametolea mfano umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kujiletea maendeleo na kusema kuwa zaidi ya vituo 300 vya Afya nchini vimejengwa na kukarabatiwa kwa kutumia nguvu za wananchi na mpango huo wa ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo mbalimbali umefanikiwa kwa kushirikisha jamii husika ambayo waratibu wake ni Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata na Halmashauri nchini.
“Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii mnalojukumu la kutumia weledi na maarifa mkiendelea kujipambanua katika katika maeneo ya taaluma na mafunzo yenu ili kutoa mchango wa umahiri wenu katika kuwezesha Familia, Jamii na Taifa kufikia azma ya maendeleo jumuishi”, amesema Dkt. Ndugulile.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Taasisi, ni muhimu kuwa na mpango wa kimkakati kuongeza mapato hivyo kutatua kero za muda mrefu hususan uchakavu wa miundombinu ya majengo na huduma za mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Ameeleza kuwa miongoni mwa maeneo ya utatuzi ni pamoja na kuimarisha matangazo ya ndani na nje ya nchi, kuimarisha mahusiano na wadau wa maendeleo, kuimarisha eneo la ushauri wa kitaalamu na kuongeza idadi ya kozi kulingana mahitaji ya vipaumbele vya kitaifa.
Mapema Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya jamii Tengeru, Dt. Bakari George akitoa taarifa kwa Mgeni Rasmi kuhusu Mahafali hayo kuwa kwa mwaka 2017/2018 idadi ya wanachuo waliodahiliwa ni 1535 ukilinganisha na wanachuo 1169 waliodahiliwa kwa mwaka 2016/2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 31 ya wanachuo.
Haya ni Mahafali ya nane kufanyika tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na jumla ya wahitimu 654 wametunukiwa vyeti katika ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada na Shahada za Uzamili wakiwa na wajibu wa kuwezesha jamii kupata majawabu thabiti ya changamoto zinazokabili

Post a Comment