Wizkid na Tiwa Savage wazua balaa

Msanii Tiwa Savage azidi kuchukua headlines kupitia mitandao ya kijamii na hii ni baada ya ngoma ya Wizkid ‘Fever’ kuachiwa rasmi  October 23,2018 ikiwa Tiwa Savage ameshiriki kama video vixen ndani ya ngoma hiyo.

Maneno yamekuwa mengi kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na video ya ngoma hiyo huku wengi wakidai kuwa wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu ingawa hawajataka kuweka wazi kuhusiana na kinachoendelea kati yao. 

Kwa upande mwingine wa mashabiki wameingilia kati na kuzungumzia   kuhusu kuvunjika kwa ndoa ya Tiwa Savage na kumuuliza kuwa haoni aibu kuwa ni mtu mzima na vitu anavyofanya pamoja na Wizkid. 

Kupitia snapchat story ya Tiwa Savage amesema “kuhusu yote hayo yaliyotajwa basi nipelekeni mahakamani au kuleni mchuzi wa pilipili na maji mengi kwasababu kwa Neema yake pekee sitoacha muda wowote”

No comments

Powered by Blogger.