Wema Sepetu: Yaani watu wametokwa na povu kama lote
Msanii wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu amewafungukia watu ambao wanasema maneno ya kashfa kufuatia kumuanika mumewe mtarajiwa, Patrick Christopher ‘PCK’.
Wema ameyasema hayo wakati akipiga stori na chombo kimoja cha habari kuwa, yeye ana uamuzi wake binafsi wa kufanya anachotaka kwenye maisha yake, lakini anashangaa watu wengine wanamuingilia mpaka kwenye maisha yake binafsi na kutokwa povu.
“Yaani watu wametokwa na povu kama lote, kisa tu mimi kumuonesha mwanaume wangu, sasa hata wakiungana dunia nzima kunisema, kama nimeshampenda watanibadilisha vipi?” alihoji Wema.
Wiki iliyopita ulizuka mjadala mzito kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram baada ya Wema kutupia picha ikimuonesha akiwa kitandani na mwanaume huyo na kuweka wazi kuwa ndiye mumewe mtarajiwa.


Post a Comment