Waziri Mkuu Ethiopia afichua Wanajeshi walivyotaka kumuua
Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema kwamba baadhi ya wanajeshi walioingia katika eneo la afisi yake wiki iliopita walitaka kumuaa.
Wakati huo, aliondoa wasiwasi uliokuwepo kwa kuwaamrisha kufanya press-ups (mazoezi ya maungo).
Abiy na wanajeshi hao walionekana wakicheka lakini aliambia bunge kwamba 'ndani yangu sikuwa na furaha'.
Katika kipindi cha miezi sita iliopita amekuwa akifanya mabadiliko muhimu na anasema kuwa baadhi ya wanajeshi wake walitaka kuzuia mabadiliko hayo.
"Maandamano hayo ya baadhi ya wanajeshi hao katika afisi ya waziri mkuu yalikuwa kinyume na sheria na hatari , kwa sababu lengo lilikuwa kusitisha mabadiliko yaliokuwa yakiendelea," Abiy aliwaambia wabunge wakati ambapo waziri mkuu anajibu maswali bungeni.
Wakati huohuo baada ya hali hiyo kudhibitiwa , baadhi ya wanajeshi walisikika wakisema: Alitoroka kabla ya sisi kiumuua.
Wengi wameshangazwa na matamshi ya waziri huyo wiki hii ambapo wiki iliopita alijibu tofauti alipoulizwa kuhusu swala hilo.
Baadaye alionekana akicheka na kutabasamu, lakini amefichua katika bunge kwamba alikuwa amekasirika na kukerwa sana.

Post a Comment