Wanafunzi waliopigwa na radi Geita waruhusiwa kutoka Hospitali



Wanafunzi 14 kati ya 21 wa Shule ya Msingi Emaco Vision waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Geita baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani wameruhusiwa kutoka hospitali 

Tukio la wanafunzi kupigwa radi mjini Geita lililotokea jana Jumatano Oktoba 17, 2018 wakati wanafunzi hao wakiwa darasani, lilisababisha wanafunzi sita kufariki dunia na kujeruhi 21 na walimu wawili. 

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Moses Simon amesema wanafunzi wengi wamepata majeraha ya miguuni na shingoni. 

Dk Simon amesema mwalimu mmoja amejeruhiwa zaidi baada ya kuungua sehemu kubwa ya mwili wake na bado wanaendelea kumpatia matibabu. 

Mwalimu wa shule hiyo, Edward Bartholomeo amesema wamesitisha kufundisha kwa muda na wataendelea na masomo Jumatatu Oktoba 22..

No comments

Powered by Blogger.