Wachezaji wawili wa Simba wafuatiliwa na vilabu vya Ubelgiji

Kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems ameweka wazi kuwa baadhi ya wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza akiwemo Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya wameanza kufuatiliwa na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji. 

Aussems ameyasema hayo kufuatia kuwa na mawasiliano ya karibu na baadhi ya wakurugenzi wa timu za Ubelgiji ambao wanafuatilia  Ligi Kuu Bara ,baada ya kuvutiwa na kiwango cha Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji. 

"Nilielezwa kwamba wengi wao wangefika hapa mwezi huu kwa ajili ya kuanza kufuatilia wachezaji ambao wataona wana viwango vya kwenda kucheza ligi ya Ubelgiji,wachezaji wapo wengi na siyo wa Simba tu. 

"Wapo wachezaji ambao wataondoka kupitia njia hii kwa kuwa wengi ni marafiki zangu na wao ndiyo waliomba hivyo  maana walikuwa tayari kuja hapa lakini watatumia njia ya mtandao kuwafuatilia wachezaji watakaowahitaji"alisema.

No comments

Powered by Blogger.