Serikali ya Zanzibar yataja mbinu itakayosaidia kukuza elimu


 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Jamii inalazimika kuwaandalia Elimu ya Maandalizi Watoto kwa lengo la kuwajengea msingi mzuri utakaowawezesha kuingia kwa kujiamini katika elimu ya sekondari na vyuo hatimaye kuwa Watumishi bora walioelimika vyema. 

Alisema Taifa linahitaji Wataalamu Wazalendo watakaoivusha Nchi katika mpito wa kuingia katika mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia yaliyoukumba ulimwengu katika Miaka ya sasa. 

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akisalimiana na Wananchi, Walimu na Wanafunzi wa Maziwa ng’ombe baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Maandalizi ya Maziwa ng’ombe Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya siku Tano Kisiwani humo.. 

Balozi Seif  alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepania kuwasaidia Vijana wake ndio maana ikaweka Elimu bila ya malipo kulikotangazwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Aman Karume Mnamo Tarehe 23 Septemba 1967. 

Aliwatahadharisha Walimu kuacha kuwachangisha fedha Wanafunzi kwa Vile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imebeba mzigo wa kugharamia Elimu Maskulini

No comments

Powered by Blogger.