Serikali yatangaza ajira zaidi ya elfu sita


Serikali kupitia Ofisi ya Rais –TAMISEMI imetangaza nafasi za kazi 6,180 katika sekta ya Afya ikiwemo Madaktari, Wafamasia, Wauguzi, Tabibu, Wahudumu wa afya nk, lengo likiwa kuhakikisha kuwa upungufu wa Watumishi wa ya afya unatatuliwa. 

Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo amekaa mbele ya wandishi wa habari na kuzitangaza fursa hizo na kusema wajitokeze watu walio na sifa za taaluma hizo za afya na kuomba nafasi hizo ili waweze kuajiriwa na kutoa huduma kwa wananchi. 

Aidha Waziri Jafo amezitaja sifa za waombaji wanazotakiwa kuwa nazo kuwa awe Raia wa Tanzania, aambatanishe nakala ya vivuli vya vyeti halisi vya kidato cha nne na cha sita, aambatanishe kivuli cha cheti cha taaluma anayoombea ajira kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) au chombo kinachotambulika na serikali kinachotoa usajili nk.

No comments

Powered by Blogger.