Je mtu ulie nae ni sahihi??
Pia ujifunze kuwa mtu mkamilifu ili uje kupata mtu alie mkamilifu. kwa hio inabidi uwe na maswali mengi kabla hujaanza kuchukua maamuzi ya kutafuta mtu sahihi.Jiulize , umekamilika au ni tamaa tu inakupeleka kutafuta mtu wa kukukampani.?
kama nia yako ni kupata mapenzi tu , basi hapo bado hujakamilika, lazima uwe na kazi kubwa ya kufanya ndani ya moyo wako kabla unahitaji kupata kazi ya kujifunza kujipenda , na kujifunza majukumu ya kupenda wengine, uwe na hisia za kujisikia mkamilifu na usalama za namba moja, yaani kupata na kutoa.
jiulize maswali yafuatayo.
1. Je ni mtu anyethubutu kujali, na ni mtu mwenye huruma na uelewa na mtu wa kukubalika na anakubali jinsi ulivyo. kukosekana kwa uelewa ni dalili ya moja kwa moja kuwa sio sahihi
2. Je anajitahidi kulazimisha ili awe sahihi?
unaweza kuwa ,mnafanya vitu kwa pamoja , lakini bado unaona kama kuna upungufu fulani kwako huyomsio mtu sahihi kwako, hata ukijitahidi vipi huwezi kufika mbali nae.
3. Je mtu ulie nae ni muwazi kiasi cha wewe kujifunza kitu kwake?
mtu muwazi ni rahisi kjifunza kujua kama anajipenda na kuwapenda wengine, lakini mtu wa kificho ni vigumu kujua , na hutaweza kujifunza kitu kwake. uwazi ni chombo cha msingi sana katika mahusiano yeyote. hata kama kuna migogoro ni rahisi kurekebisha baina yenu . lakini watu wenye kificho ni ngumu hata kama kuna migogoro wanakuwa na hasira , hufoka , huhamaki, wanakuwa na hisia kali za kimwili zaidi. kwa hio sio sahihi.
4. Mnashirikiana katika kipato chenu?
mnakubaliana katika matumizi?, uzazi, kula manunuzi ya vitu, mazoezi,usafi na kuwajibika kwa pamoja na mnaelewana?.
5. Unapata zile hisia za msingi , zile cheche zinazokuvuta kwake? unapenda kuwa karibu nae? unapenda jinsi alivyo?
Inawezekana ana harufu fulani hupendi, kama huna hizi hisia ndani ya miezi 6 ya kuwa na huyo mtu basi hakufai, uelewe huyo ni rafiki tu wa kupita hawezi kuwa mwenza wa maisha
Post a Comment