Polisi wamthibiti aliyetaka kuingia Ikulu kwa lazima Marekani


Polisi wa Marekani wanaolinda Ikulu ya White House walilazimika kufyatua risasi usiku wa jana  ili kuthibiti mwanaume aliyekuwa akijaribu kuingia kwenye ikulu hiyo kwa lazima. 

Mwanaume huyo alikimbia kuingia sehemu yenye ulinzi mkali muda mfupi baada ya Rais Trump kusubiri ndege ya helicopter kutoka eneo hilo akienda ziara ya kigeni nchini Uingereza. 

Maafisa wa polisi wanaolinda White House walisikika wakionya mwanaume huyo kabla ya kufyatua risasi, hata hivyo haijabainika hali ya mshukiwa baada ya tukio hilo.

No comments

Powered by Blogger.