Namna sahihi ya kuongeza kipato chako mara mbili zaidi ya hapo ulipo sasa
Suala la kuongeza kipato ni la msingi sana na lina umuhimu mkubwa kwa kila mmoja. Si watu wengi sana duniani wana kipato cha kutosha kutimiza ndoto zao maishani,wakati mwingine hata kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula,malazi,mavazi ,afya na elimu binafsi na za watoto wao.
Kama ilivyo kwangu binafsi naamini pia kuna umuhimu mkubwa wa kuangalia namna nyingine tofauti na kile unachokifanya sasa hivi ambacho kitasaidia kuongeza kipato juu ya kile unachopata sasa.
Mbinu za Kuongeza Kipato Kwa Asilimia 100 au Zaidi ya Kipato Chako cha Sasa
Zifuatazo ni mbinu ambazo zinaweza kumsaidi kila mmoja anayetaka kuongeza kipato chake
1. Anzisha Biashara yenye Mahitaji kwa Jamii
Zig Ziglar ,Mwandishi wa vitabu na mwanamasoko maarufu duniani anasema “ukiwasaidia watu wengi kupata wanachotaka nawe pia utapata unachotaka”. Kwa maana nyingine ni kwamba ukitaka kufanikiwa kiuchumi basi tafuta nini watu wanataka na tengeneza bidhaa au toa huduma kujaza mahitaji hayo ya watu.
Kwahiyo unaweza kuongeza kipato chako kwa kuanzisha biashara inayotoa suluhisho la matatizo ya watu au huduma inayohitajika na watu.
Kama watu wanahitaji kupunguza uzito kutokana na hatari za kiafya hivyo wangependa kupata suluhisho ya tatizo lao,hivyo unaweza ukaanzisha huduma ya mazoezi kwa kuanzisha nyumba ya mazoezi pamoja na kuweka walimu wa kuwasidia wateja wako. Wateja wanaweza kujisajili na kulipa ada ya mwaka ya uanachama ili kuhudhuria mazoezi au wakalipa kila wanapohudhuria.
Au unaweza ukaanzisha duka la vyakula vyenye kujenga afya njema kama mbogamboga na unga wa nafaka zisizokobolewa,mafuta yasiyo na rehemu nyingi kama alizeti na ufuta na vyakula vingine visivyo na madhara kwa afya za watu.
2. Ongeza Mtandao wa Watu na Mahusiano
Unaweza kuongeza kipato chako kwa kujenga mtandao na watu mbalimbali na kisha kuwajulisha biashara unazofanya. Wataalamu wa masoko wanasema watu hawanunui bidhaa au huduma yako unayotoa bali wananua mahusiano. Kwa maana kwamba watu ili wanunue bidhaa yako au huduma ni lazima wawe na mhusiano mazuri na wewe kwanza. Mahusiano haya yanaweza kuwa yamejengwa kwa muda mrefu au katika dakika chache mtu alipoingia dukani kwako.
Vitu 3 vinavyomfanya mtu anunue bidhaa yoyote:
Imetambulika kuwa ili mtu anunue kitu vifuatavyo ni vitu muhimu
.Utaalamu : Aamini kuwa wewe mtoa huduma ni mtaalamu katika eneo hilo
.Urafiki : Mahusiano yenu ni mazuri yani umejenga urafiki mfano kwa huduma kwa mteja unyoionesha na lugha nzuri unayotumia kwa mteja, watu wanannnua toka kwa watu wanaowapenda
.Uaminifu au Imani : Mtu anayenunua ni lazima aamini kuwa mtu anayempa huduma ana uwezo na ni mkweli.
Mambo haya matatu ni muhimu sana kusaidia kufanikiwa katika utoaji wa huduma na mapato ya biashara unayotoa.
3. Tangaza Biashara Zako katika Mtandao
Matangazo ya biashara ni muhimu sana ili kuwafikishia habari watu wengi. Kuna aina nyingi za kuweza kutangaza biashara kama redio,TV na magazeti lakini hapa tutaangalia aina mpya na yenye nguvu kubwa ya matumizi ya mtandao wa intaneti. Imefahamika kuwa takribani watu bilioni 3 (Kulingana na taarifa toka mtandao wa internetworldstats.com Nov 2015) wapo katika intaneti kwa maana ya kuwa watu hawa wanatumia mtandao wa intenet aidha kwa mawasiliano,burudani au biashara. Katika hawa wengi wapo katika mitandao ya kijamii kama facebook Bilioni 1 , Twitter Milioni 400 na Instagram Milioni 100.
Kama unataka kuwafikia watu wengi zaidi duniani basi mtandao wa intaneti ni sehemu ya kufikiria kwanza.
Baadhi ya matangazo katika intaneti yanalipiwa. Na mengine ni bure. Andaa matanzano ya video na weka katika mitandao ya facebook,youtube na picha katika mitandao ya picha kama intragram an pinterest.
Tovuti na blogu ni kitu kingine ambacho ni muhimu sana nadiriki kusema cha lazima katika karne hii ya habari.
Bill Gate (Tajiri namba moja Duniani kwa muda mrefu) aliwahi kusema “Kama biashara yako haitakuwa katika intaneti basi biashara yako itakufa” akiwa na maana kuwa ni muhimu sana kwa biashara yoyote kujitangaza na kuwa katika mtandao wa intaneti katika karne hii ya digitali. Watu wataendelea kuwa digitali zaidi na huduma nyingi zitakuwa katika mtandao.
Inatabiliwa kuwa katika karne ijayo hata hela zitakuwa katika mfumo ywa kadi na eletroniki tu. Unaweza kuona haya yameshaanzakutokea. Kadi za plastiki zinatumika kununua huduma mbilimbali na huduma za kieletroniki kama “mobile money” na “web wallet” ambapo huhitaji hata kuwa na kadi wala pesa taslimu kufanya miamala.
Hivyo ili kuoneza kipato tangaza huduma unazitoa kupitia mtandao na jenga biashara yako katika mtandao
Ukitaka habari zaidi kuhusu kutengeneza tovuti na kuiweka biashara yako katika mtandao kwa gharama ndogo pata msaada kwa kuwasiliana na Absolute Solutions Ltd – Bofya Hapa
4. Ongeza Elimu na Utaalamu katika Kazi
Unaweza kuongeza kipato zaidi kwa kuboresha kili unachofanya sasa. Mfano kama wewe umeajiriwa basi unaweza kupata malipo zaidi kwa kukuza ujuzi wako na kupandishwa cheo na kulipwa mshara mkubwa zaidi.
Jenga uwezo wa kuweza kufanya vizuri zaidi na kuzalisha zaidi ili kuweza kupata malipo maradufu.
Anza kozi katika muda wa jioni au kozi ya mbali. Lakini uanaweza kwenda chuoni na kusoma kwa masaa yote kama unaweza kupata ruhusa hiyo kazini kwako.
Kama umejiajiri na unafanya bishara binafsi ni muhimu kujifunza kitu kipya na kupata taaluma zaidi ambayo itakusaidia kuboresha biashara yako na kuongeza mapato.
Natumaini makala hii itakusaidia katika maamuzi yako kuhusu kuongeza kipato kwa asilimia 100 ya kile unachopata sasa na kuboresha maisha yako na familia yako.
Tafuta matatizo ambayo watu wanayo na yanahitaji ufumbuzi,buni na jenga suluhisho litakalowasaidia watu na matatizo yao na utafanikiwa kuongeza kipato chako wakati ukiwasaidia watu katika matatizo yao.
Post a Comment