Mambo mawili yatakayo weza kuku saidia katika mahusiano ya kimapenzi

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.” 

Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi. 

Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea,yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana. 

Yafutayo ndiyo mambo ya msingi ili uweze kudumu katika mahusiano ya kimapenzi: 

Uaminifu 
Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. 

Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako. 

Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. 

Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli mara zote. Ongeeni juu ya mipango na mawazo yenu bila kufichana. 

Watambulishe kwa mpenzi wako ndugu ,jamaa na marafiki wakaribu ili kumpa mwenza wako amani. 


Weka muda kwaajili ya Mwenza wako. 
Mahusiano mazuri kati ya wapenzi yanahitaji muda wa wapenzi hao kukaa pamoja. Wapenzi wasio na muda wa kukaa wana hatari ya kupoteza mvuto wa mahusiano yao na hivyo kuhatarisha uhai wa mapenzi kati yao. 

Kama wapenzi wapo mbali mbali basi wanahitaji kuweka muda wa kuongea kila inapowezekana. 

Tafuta muda wa kutoka pamoja,hata kama mtaenda mkahawani kunywa chai au juisi tu,inatosha sana na inawaweka karibu zaidi. 

No comments

Powered by Blogger.