Korea Kaskazini huenda ikavunja mazungumzo na Marekani kuhusu Nyuklia


Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Choe Sun-hui amesema kiongozi wao Kim Jong-un anaweza kuvunja mazungumzo ya kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia na rais wa Marekani na kusema Marekani imepoteza "nafasi ya dhahabu" 

Mkutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ulimalizika bila kufikia makubaliano baada ya Marekani kukataa kutoa nafuu ya vikwazo kwa Korea Kaskazini. 

Itakumbukwa kuwa mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili, uliofanyika nchini Singapore mwezi Juni mwaka 2018, ulikosolewa kwa kutofikiwa kwa matarajio, hali iliyoleta hali ya kukisia kuwa Trump atashawishi kufanikisha hili katika mkutano wa Hanoi kufikia makubaliano ya kukomesha zana za nuklia.

No comments

Powered by Blogger.