Ijue kanuni halisi ya Ubongo wako unavyofanya kazi

Watalamu mbalimbali wa masuala ya mafanikio wanasema ya kwamba kanuni ya akili yako inatokana na ubongo wako, na katika ubongo wako unafanya kazi kutokana na  mawazo yako ambayo kila siku unakuwa unayawaza. Swali dogo la kujihoji ni je kwa kila siku huwa unawaza nini? 

1.      Je mawazo yako huwa ni chanya? 

2.      Au mawazo yako huwa ni hasi? 

Kama mawazo yako ni chanya ni hatua gani amabazo umekwisha zichukua mpaka sasa ambazo kimsingi umekuwa ukijivunia? Majibu naomba ubaki nayo maana wewe ndiye ujuaye. 

Nawe ndugu yangu ambaye kimsingi kwa namna moja ama nyingine umekuwa ukiwaza mawazo hasi, swali dogo ambalo unatakiwa kujiuliza kwanini umewekeza nguvu na akili zako katika kufikiri vitu hasi ? naomba nawe mwenye tabia hii ufanye tafakari kisha naomba majibu usinipe. 

Nimeanza kwa tafakari  hiyo fupi ili tuone kwa pamoja akili zetu tumezielekeza wapi zaidi? Na akili hizo hizo zinatupa matokeo gani ambayo yapo katika maisha yetu ya kila siku? Kwa kuwa kama nilivyowahi kueleza hapo awali ni kwamba kanuni ya akili inasema ya kwamba wewe ni matokeo ya mawazo yako, hii ikiwa na maana kila ambacho unakiwaza katika mawazo yako ndicho ambacho kinachotokea katika hali halisi. 

Hivyo kama mawazo yako ni hasi, basi hata kile utakochokifanya basi matokeo yake yatakuwa ni hasi, kama unawaza kutajirika kwa kuwa jambazi basi matokea yake ni jiandae kufungwa. Maana akiwazacho mtu ndicho kitakochomtokea. 

Mwisho nimalize kwa kusema ya kwamba kama kweli umechoka hali uliyonayo hususani masuala ya umaskini, jitahidi ufuate mfumo wa kufikiria chanya kila wakati. Maana matokeo ya mawazo chanya ni mafanikio ya kweli. 

Asante kwa kusoma makala hii naomba uwaze kuwa bora kwa kuwa na mawazo chanya kila wakati, kwani ukiwa hivyo mafaniko makubwa yanakuja kwa upande wako. 

No comments

Powered by Blogger.