Fahamu ugonjwa wavkuvimba macho kwa kuku na jinsi ya kutibu

Ugonjwa wa kuvimba macho kwa kuku ni miongoni mwa magonjwa ambayo chanzo chake mara nyingi hutokana na mfumo wa hewa. Haya ni magonjwa ambayo ni sugu na huwaathiri kuku kwa kiwango kikubwa sana. 

Sasa tuone chanzo cha ugonjwa huu wa kuvimba macho 
• Maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha kuku wagonjwa na kwenye vimelea 
• Kupitia mfumo wa hewa kutoka kuku wagonjwa 
• Kupitia mayai, hivyo maambukizi huendelea kutoka kizazi hadi kizazi 

Dalili za ugonjwa huu ni; 
• Kuku kukoroma 
• Kuku hutoa makamasi 
• Kuku wanakohoa kwa muda mrefu, wiki hadi mwezi 
• Kuvimba macho 
• Kutingisha kichwa 
• Vivo vya kuku viaweza kufikia hadi asilimia 20 Uchunguzi 
• Kamasi nzito zenye usaha zilizotapakaa kwenye pia, koromeo, mapafu na vifuko vya hewa 

Jinsi ya kutibu ugonjwa huu. 

• Madawa aina ya sulfa na antibiotiki 
• Kwa ushauri zaidi  waone watalamu wa vifugo ili wakupe maelekezo kamili 

No comments

Powered by Blogger.