Mjaslia mali lazma ajali mambo haya
Habari rafiki mpenda maendeleo, natumaini unaendelea vizuri na mapambano ya maisha. Nikutie tu moyo, endelea na harakati hizo, naamini ipo siku utaona matunda ya unachokifanya. Kama kawaida leo nakuletea makala nyingine, hii ni juu ya sifa za mjasiriamali.
Kuna watu wengi sana wanajiita wajasiriamali lakini kiuhalisia si wajisiriamali. Hii imenifanya nifikirie juu ya hili.
Zifuatazo ni sifa za mjasiriamali. na kama huna sifa kati ya hizi basi hujawa mjasiriamali wa ukweli bali utakuwa unabip tu.
Awe na malengo
Hii ni sifa kubwa ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwa nayo, kwanza lazima uwe na malengo uliyojiwekea kwamba unataka kufikia wapi katika biashara yako. Kama ni kuwa na pesa nyingi sema unataka kiasi gani kabla ya mwaka kuisha. Kwa mfano; nataka kabla ya mwaka 2016 kuisha niwe nimetengeneza Million 20. Hii itakufanya ufanye kazi kwa bidii ili ufikie malengo hayo.
Awe ni mtu asiyekata tamaa
Mjasiriamali yeyote duniani ni mtu ambaye si rahisi sana kukata tamaa katika kazi zake, watu wengi sana wamekuwa na malengo makubwa lakini wanashindwa kuyafikia kwa sababu wanakata tamaa mapema sana, hii huwafanya warudi nyuma. Mfano, Mtu aliyeajiriwa anakuwa na malengo ya kujiajiri, anaanzisha biashara, asipopata faida kama alivotarajia hukata tamaa na kutamani tena kuajiriwa na hatimaye kutafuta ajira tena. Nikutie moyo tu, hakuna kitu kinachokuja kwa urahisi kama unavyofikiria. Kaza buti, songa mbele, changamoto ni chachu ya mafanikio.
Awe ni mtu wa kujiamini.
Siku zote anayejiamini ndio hupata mafanikio kwa urahisi. Watu wengi wamekuwa wakishindwa katika biashara zake kwa kushindwa kujiamini, kumbuka hiyo ni biashara yako, acha kuangalia watu wanasema nini, wewe endelea na harakati zako ipo siku hao wanaokubeza watakusifia.
Ajali muda
Muda ni kitu kidogo sana lakini muhimu kuliko kitu chochote. Mbaya zaidi dakika moja au hata sekunde moja ikipita hutakutana nayo tena katika mzunguko wa maisha yako tena, kwahiyo kama umekuwa na malengo ya kufanya kitu fulani, basi fanya haraka iwezekanavyo, ukizidi kuchelewa unaendelea kuweka matatizo na vikwazo katika kazi yako au hata biashara yako. Kuna msemo unasema “muda ni mali” au “time is money”.
Misemo hii imefananisha muda na pesa, kwa sababu pesa ni kitu muhimu lakini utapata pesa kwa kutumia muda vizuri, acha kuahirisha mambo mara kwa mara, fanya maamuzi sasa, kesho kamwe haitafika.
Awe na kauli njema, tabasamu na nadhifu
Hii ni nguzo muhimu sana kwa mjasiriamali, unapokuwa na kauli njema na mwenye tabasamu na nadhifu unapokuwa unahudumia mteja unavutia wateja wengi zaidi, na kama utakuwa na kauli mbaya na mchafu wateja wanakimbia na mwisho wa siku unaanza kufikiri umerogwa, kumbe wewe ndiye mchawi namba moja wa biashara yako. Zingatia hilo na utaona unavyopata wateja kuliko kawaida.
Post a Comment