VIDEO: MO APATIKANA AKIWA HAI

Taarifa zilizotufikia leo Octoba 20 mwaka huu zinaeleza kuwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo Dewji) amepatikana akiwa salama.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amethibitisha kuonekana kwake na kusema kuwa watekaji walimchukua na gari ile ile ambayo wamtekea na kwenda kumtupa viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.

"Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri."

Aidha taarifa za awali ambazo zilidhibitisha kupatikana kwake ambapo uliandikwa ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter wa kampuni yake, amesema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama."

Ujumbe huo umeandikwa saa tisa na robo alfajiri, na umeelekezwa kwamba umeandikwa kutoka Dar es Salaam.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

No comments

Powered by Blogger.